• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI IMETOA MBEGU ZA PARETO BURE KWA WAKULIMA MKOA WA SONGWE

Posted on: October 26th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Songwe,Mhe. Dkt. Francis K. Michael, ameipongeza serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutenga TZS 200 Milioni kusaidia sekta ya kilimo kufanikisha utafiti wa zao la Pareto kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) Kituo cha Uyole. Dkt. Michael ameonesha furaha yake kuhusu hatua hii muhimu, hasa kwa kuinua sekta ya kilimo, ikiwemo zao la Pareto ambalo kwa muda fulani lilisahaulika. Amesisitiza kuwa Mkoa wa Songwe una uwezo mkubwa wa kuzalisha tani 12,000 za maua makavu ya Pareto, na hii ni fursa kubwa ya kuboresha uchumi wa Mkoa wa Songwe


Katika kufanikisha jitihada hizi, Kituo cha Utafiti wa Mazao ya Kilimo TARI Kituo cha Uyole kimefanya utafiti wa mbegu za Pareto. Mkurugenzi wa Bodi ya Pareto nchini, Lucas Ayo, alisema kuwa serikali imetoa TZS 200 Milioni  kwa ajili ya utafiti zaidi katika zao hilo. Utafiti huu unatarajiwa kuboresha ubora na uzalishaji wa Pareto nchini.


Kwa kuzingatia umuhimu wa kuongeza uzalishaji wa zao la Pareto nchini Tanzania, serikali imetangaza mpango wa kutoa kilo 2,000 za mbegu za Pareto bure kwa wakulima katika nchi nzima. Katika jitihada za kuimarisha uzalishaji wa zao hili, Mkoa wa Songwe, na hasa Wilaya ya Ileje, umepokea gawio la kilo 260 za mbegu hizi. Hatua hii inatarajiwa kusaidia kuongeza uzalishaji wa Pareto na kufikia lengo la kuzalisha tani 1,000 za maua makavu ya Pareto kwa msimu mmoja.


Ni muhimu kutambua kuwa Tanzania ni nchi pekee katika bara la Afrika inayolima Pareto, na ni nchi ya pili duniani kwa uzalishaji wa zao hili. Zaidi ya hayo, Tanzania inajulikana kwa kuzalisha Pareto yenye ubora wa hali ya juu, na uzalishaji wake kuu unafanyika katika mikoa ya nyanda za juu kusini. Hii ni habari njema kwa wakulima na wafanya biashara katika kukuza uchumi wa mkulima na  taifa kwa ujumla kupitia sekta ya kilimo .

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI January 30, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YA SAINI MRADI WA ZAIDI YA BILIONI 119.9 UJENZI WA MRADI WA MAJI TUNDUMA VWAWA

    March 20, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA ILEJE MHE. FARIDA MGOMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA AFUNGUA HUDUMA YA WIKI YA SHERIA MKOANI SONGWE

    January 25, 2025
  • TASAF MKOA WA SONGWE IMEFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI NA KUJIONEA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANUFAIKA WA TASAF MOMBA

    January 03, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO MKOANI SONGWE.

    November 07, 2024
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras@songwe.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.